Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yashinda kibabe kwa Mkapa, Kagere afanya ukatili

FDSaejNXEAEFV8n (600 X 643) Wachezaji wa Simba wakimpongeza na kushangilia goli la ushindi la Meddie Kagere

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama masihara lakini wameondoka na alama zote tatu dakika ya mwisho kabisa ya mchezo.

Baada ya piga nikupige ya dakika zote Bull Straika, Meddie Kagere amefunga goli ambalo limeamsha hisia za mashabiki kila pembe ya nchi.

Ndani ya dimba la Mkapa huku wakitawala sehemu kubwa ya mchezo Simba imeondoka kifua mbele baada ya kuichapa Namungo FC kutoka Lindo kwa goli 1-0.

Namungo ambao walikua pungufu baada ya mchezaji wao kuonyeshwa kadi nyekundu dakika za mapema kipindi cha pili na wakajitahidi kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live