Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yapigwa bao tuzo za Ligi Kuu

Simba Tuzo Kikosi cha Mnyama, Simba SC

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati watani wao Yanga wakizidi kupeta katika tuzo za mchezaji bora wa mwezi na kocha bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya NBC, mambo yameonekana kuwa magumu kwa Simba msimu huu.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi hiyo, katika msimu huu hawajatoa mshindi wa tuzo yoyote kati ya hizo mbili ambazo zimeshatolewa kwa miezi sita sasa.

Kwa upande wa mchezaji bora wa mwezoi, nyota wa Polisi Tanznaia, Vitalis Mayanga ndio alianza kufungua dimba kwa kuibuka mshindi, Septemba na mwezi uliofuata akliyeibuka kinara alikuwa ni nyota wa Yanga, Feisal Salum.

Mwezi Novemba, mshindi alikuwa ni Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons, akafuatiwa na Reliants Lusajo wa Namungo FC, aliyeibuka mshindi Disemba, Fiston Mayele akatwaa ya mwezi Januari huku mwezi uliopita ikienda kwa Saido Ntibazonkiza.

Kwa upande wa kocha bora wa mwezi, aliyeanza kutwaa msimu huu alikuwa ni Malae Hamsini wa Polisi Tanzania, mwezi Oktoba ikaenda kwa Nasreddine Nabi wa Yanga na kisha mwezi Novemba ikatua kwa Salum Mayanga ambaye wakati huo alikuwa akiinoa Tanzania Prisons.

Aliyekuwa kocha wa Coastal Union ambaye kwa sasa ameachana na timu hiyo, Melis Medo aliibuka mshindi mwezi, Disemba akifuatiwa na Francis Baraza aliyetwaa tuzo mwezi Februari na mwezi uliopita ilitua mikononi mwa Nabi ikiwa ni ya pili kwake msimu huu.

Kwa upande mwingine, meneja wa Uwanja wa Azam FC, Sikitu Kilakala ameonekana kutamba katika tuzo ya meneja bora wa mwezi wa Uwanja.

Kilakala ameibuka mshindi mara tatu tofauti akifanya hivyo katika miezi ya Novemba, Disemba na Februari.

Washindi wengine wa tuzo ya meneja bora wa mwezi wa uwanja ni Tumaini Ikomba wa Uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Black Rhino aliyetwaa mwezi, Septemba, Modestus Mwaluka wa Uwanja wa Sokoine aliyekuwa mshindi mwezi Oktoba na John Nzwalla wa Uwanja wa Nelson Mandela aliyeshinda mwezi Januari.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz