Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeipiga faini ya milioni 1 klabu ya Simba SC kwa kosa la mashabiki wake kumwaga vitu vyenye asili ya unga katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kabla ya wachezaji hawajaanza kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo. Tukio hilo limetafsiriwa kama vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa klabu.