Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yapelekwa Kaitaba

Kaitaba Stadium Simba yapelekwa Kaitaba

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ni rasmi mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Kagera Sugar na Simba utapigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera Desemba 21 baada ya uwanja huo kudhibitishwa kufunguliwa kwa ajili ya kutumika.

Akizungumza Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Ally Masoud alisema walipokea barua rasmi juzi kutoka Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya kuruhusu uwanja wao kutumika kwenye michezo ijayo.

“Tumeambiwa tutaanza kuutumia kuanzia Disemba 11 ila mchezo wetu ujao na Ihefu tutaocheza Desemba 2 tutaendelea kuchezea CCM Kirumba kama tulivyokuwa tunachezea awali,” alisema.

Masoud alisema uwanja wa Kaitaba haukufungiwa kama inavyoelezwa isipokuwa wamiliki wao wa uwanja huo walikuwa wanautumia kwenye mbio za Mwenge Kitaifa zilizoanza Agosti Mosi hadi Oktoba 14.

“Baada ya mbio hizo kuisha (TPLB) ilitaka kwanza wakaguzi waje kuukagua kama unakidhi kuendelea kutumika au laah! na tunashukuru wamekuja wamejiridhisha na hilo,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti