Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yapaa na matumaini CAF

70642 Simba+caf+pic

Fri, 9 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI cha Simba kimeondoka nchini leo Ijumaa saa 12:00 asubuhi kuelekea nchini Msumbiji ambapo watakwenda kucheza mechi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wapinzani wao UD Songo.

Kikosi hicho cha Simba kiliondoka na wachezaji 19, benchi la ufundi na viongozi huku wachezaji nane wakibaki kuna ambao walikuwa majeruhi kama Ibrahim Ajibu, Wilker Da Silva na Aishi Manula, wakati Haruna Shamte, Miraj Athuman, Said Ndemla, Yusuf Mlipili na Kennedy Juma walibakishwa kutokana hawakuwa katika mipango ya mechi hiyo.

Wachezaji waliondoka Benno Kakolanya, Shomary Kapombe, Gadiel Michael, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Sharaf Eldin Shiboub, Francis Kahata, Meddie Kagere, John Bocco, Clatous Chama, Ally Salim, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Tairone Da Silva, Mzamiru Yassin, Gerson Vieira, Deo Kanda, Hassan Dilunga na Rashid Juma.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems alielezea licha ya kuwafuatilia kwa muda mrefu wapinzani wao katika mechi zao za Ligi ya Mabingwa Afrika ilibidi aende mtu kuwaangalia ili kumpa taarifa zaidi za kiufundi kabla ya kukutana nao katika mechi ya kwanza.

"Nimekuwa nikiwafuatilia kwa muda mrefu lakini timu zinabadilika, na wachezaji wanabadilika, hivyo jana Alhamisi kuna mtu alienda kuwaangalia katika mchezo waliocheza wao kule kwao na kuona baadhi ya mambo ambayo nitayatumia katika mchezo huu wa kesho ugenini," alisema Aussems.

Chanzo: mwananchi.co.tz