Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamuita Kakolanya...

Beno Kakolanya Bb Makipa wa Simba

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kumekuwa na fununu nyingi juu ya kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya kutakiwa na timu kadhaa za ndani na nje ya nchi wakati mkataba wake ukielekea ukingoni na fasta mabosi wa klabu hiyo wamefanya jambo kwa kumuita kipa huyo mezani ili kuzungumza naye.

Simba imeamua kukaa mezani na Kakolanya aliyewahi kuzichezea Tanzania Prisons na Yanga, kwa nia ya kujadiliana juu ya kumpa mkataba mpya mara watakapoafikiana.

Habari za ndani kutoka kwa mtu wa karibu na Kakolanya, zinadai baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, walimuita kipa huyo huyo na kuzungumza naye wakimuwakilisha mwenyekiti wao, Salim Abdalah ‘Try Again’ aliyekuwa bado hajarudi nchini na mchezaji akiwa keshaingia kambini Jumanne iliyopita.

Try Again , aliyewasili siku hiyo na kukuta tayari baadhi ya wajumbe wa bodi wameshakaa na Kakolanya na kutaka kufahamu msimamo wake.

Chanzo hicho kililiambia Mwanaspoti, katika majadiliano hayo wajumbe walimuambia kipa huyo, Simba ipo tayari kumpa Sh 60 milioni, lakini Kakolanya aliwataka waongezewe mzigo.

“Walikaa lakini sio kwa muda mrefu kwani sababu kubwa ilikuwa kutaka kujua anachokitaka mchezaji ili waone wanamalizanaje,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Wajumbe walitaka kumpa mkataba wa Sh60 milioni, ila jamaa akitaka Sh100 milioni, hivyo kushindwa kumalizana na kuahidiana kukutana tena baada ya mechi ya jana.”

Chanzo hicho kilisisitiza; “Kakolanya kwa misimu miwili inayomalizika alisaini kwa fedha ileile bila kupanda ila aliongezewa mshahara na yote wajumbe walidai hachezi, ila kwa sasa jamaa hayupo tayari kwani amecheza na ameonyesha kiwango.”

Kakolanya juzi wakati akijiandaa na mchezo wa michuano ya CAF dhidi ya Raja aliliambia Mwanaspoti; “Ni kweli mkataba wangu na Simba umebaki miezi michache, lakini siwezi kuongea lolote.”

Habari za uhakika Kakolanya kwa muda mrefu anasakwa na Azam kabla ya Singida Big Stars nayo kuingia kwenye mbio hizo. huku pia zikitajwa klabu kutoka Uarabuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live