Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamuacha Lawi Dar, yatoa kauli nzito

Lawi Ally Salim Msz Simba yamuacha Lawi Dar, yatoa kauli nzito

Mon, 8 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba ikipaa pipa jioni ya leo kuelekea Misri kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2024-2025, beki Lameck Lawi yupo zake Dar es Salaam na kikosi cha Coastal Union akijifua tayari kwa michuano ya Kagame huku mwenyewe akisema yeye ni mchezaji halali wa Coastal Union.

Lawi ambaye alikuwa wa kwanza kutambulishwa ndani ya Simba kwa mastaa wao wapya kuelekea msimu ujao, inaelezwa dili hilo limekufa kutokana na kukiukwa utaratibu wa usajili wake.

Akizungumza na wanahabari wakati kikosi hicho kinaondoka nchini, Meneja wa Habari na Mawasilinao wa Simba SC, Ahmed Ally amesema sakata la Lawi litaamriwa na mamlaka za sheria za soka.

“Vitasa tulio nao kwa sasa ni Che Malone Fondoh, Karabpou Chamoka, Abdulrazak Hamza na Hussein Kazi, hao ndiyo mabeki wanne wa kati wa Simba tulio nao. Kuhusu Lameck Lawi tumemsajili tukampa pesa na timu yake tukaipa pesa lakini yametokea ya kutokea.

“Mambo yake yatakwenda kumalizwa na mabaraza ya kisheria itavyoamriwa Simba Sc tunaendelea na maisha yetu,” amesema Ahmed Ally.

Kwa upande wake, Lawi amesema ni kweli yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kambi kujiandaa na michuano ya Kagame inayotarajiwa kuanza kesho Jumanne.

"Ndio nipo Dar es Salaam na Coastal Union kwa sababu ni mchezaji wa hii timu, tumekuja hapa kwa ajili ya kambi tunajiandaa na michuano ya Kagame," alisema Lawi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live