Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamtambulisha Luis wa UD Songo

90739 Pic+simba Simba yamtambulisha Luis wa UD Songo

Fri, 3 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Yametimia! Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba imejibu mapigo kwa Yanga baada ya leo kumtambulisha kiungo wa kimataifa wa Msumbuji, Luis Jose Miquissone akitokea UD Songo.

Simba imemtambulisha kiungo Miquissone leo mchana ikiwa ni saa 24 tu baada ya watani zao Yanga kumtambulisha kiungo Haruna Niyonzima kutoka AS Kigali jana.

Usajili wa nyota hao wawili unaongeza radha ya mechi ya watani wa jadi itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa kwa Simba kuikaribisha Yanga.

Kiungo huyo Luis amekabidhiwa jezi na kocha Sven Vandenbroeck tayari kujiunga na kambi ya mabingwa hao wanaojianda na mechi yao ya kesho.

Simba imemsajili Miquissone baada ya kiungo huyo kuonyesha soka la kiwango cha juu pamoja na kufunga wakati timu ya UD Songo ilipoitoa Simba katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Kabla ya kusajiliwa na Simba kiungo huyo wa kimataifa wa Msumbuji alikuwa akihusishwa kutakiwa na Yanga, lakini dakika za mwisho miamba hiyo ya Msimbazi ilifanikiwa kuipata saini yake.

Kiungo Miquissone aliwasiri nchini usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere akitokea Ethiopia alipounganishiwa ndege akitokea kwao Maputo.

Asubuhi ya leo alikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa katika ofisi ya timu hiyo zilizopo Posta na kusaini mkataba.

Luis aliyezungumza na Mwanaspoti akiwa Maputo kabla ya kuanza safari alisema; “Nikifika Ethiopia nitalazimika kusubiri ndege nyingine ambayo nitaunga hapo kuja nayo Tanzania na nitafika saa 9:00 alfajiri ya Ijumaa na kiongozi mmoja wa Simba atakuja kunipokea,” alisema

“Nakuja huko Tanzania moja kwa moja na nikishasaini mkataba ambao tulikubaliana, nitaanza kazi huku nikisubiri mambo ya msingi ambayo tulikubaliana awali, nyumba nzuri ambayo nitaishi na gari ya kutembelea katika mizunguko yangu ya kila siku.

“Sina wasi wasi kwamba nitakutana na presha kutoka katika timu nyingine kwa kuwa nilishindwa kwenda kwao, kwani Simba ndio walikuwa wa kwanza kunifuata ila hawakuendelea lakini hata ofa yao ambayo wamenipatia wakati huu ni kubwa nisingeweza kuacha,” alisema Luis atakayekuwa jukwaani Taifa Simba ikikwaruzana na Yanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz