Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamshushia mvua ya magoli Tabora United 4-0

Simba Yamshushia Mvua Tabora Simba yamshushia mvua ya magoli Tabora United 4-0

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC imemshushia kichapo cha goli 4-0 Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Magoli ya Simba yaliwekwa kimiani na Pa Omary Jobe, Sadio Kanoute, Che Marone na Fredy Michael.

Simba imefikisha alama 29 kwenye msimamo wa Ligi Kuu akiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo nyuma ya Azam FC wenye alama 31 na Yanga SC ambao wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama zao 34.

Yanga na Azam tayari wamecheza michezo 13 huku Simba wakiwa wamecheza michezo 12.

Simba anatarajia kucheza na Azam FC Februari 9, 2024 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live