Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamshushia mvua ya magoli Azam FC

Simba Vs Tabora.jpeg Simba yamshushia mvua ya magoli Azam FC

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Magoli ya Sadio Kanoute, Fabrice Ngoma na David Kameta 'Duchu' yametosha kulizamisha jahazi la Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa Mei 9, 2024 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Simba wameondoka na alama zote tatu na ushindi huo wa 3-0 katika mechi ambayo kipindi cha kwanza ilikuwa na ushindani mkubwa na Azam FC kukosa nafasi nyingi za wazi ikiwemo penalti waliyoipata na Feisal Salum 'Fei Toto' kushindwa kumfunga Ayoub Lakred.

Simba sasa imefikisha alama 56 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC huku Azam wakisalia na alama zao 57 wakiwa mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya Simba.

Mchezo mmoja alio nao Simba mkononi ni dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Mei 12 katika uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC ambao Simba walikuwa wenyeji, walilazimishwa sare ya 1-1 baada ya Simba kusawazisha dakika za jioni kupitia kwa faulu aliyoipiga Clatous Chota Chama.

Kwenye mchezo huo wa mkondo wa kwanza, Azam walipata goli lao kupitia kwa mshambuliaji wao Prince Dube.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live