Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamalizana na vyuma hivi

Mutaleee Joshua Simba yamalizana na vyuma hivi

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba inatajwa kukamilisha usajili wa nyota wa kwanza wa kigeni, winga Joshua Mutale kutoka klabu ya Power Dynamos ya Zambia.

Simba ilituma maafisa wake nchini Zambia kwa ajili ya kukamilisha usajili huo wa winga huyo kinda mwenye umri wa miaka 22 tu.

Mutale anakuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kusajiliwa na Simba katika dirisha hili la usajili ambalo limefunguliwa rasmi leo.

Aidha taarifa za ndani zimethibitisha kuwa Simba pia imeshakamilisha usajili wa wachezaji wawili wa ndani beki Lameck Lawi kutoka Coastal Union na kiungo Yusuph Kagoma kutoka klabu ya Singida Fountain Gate ambayo kuanzia msimu ujao itafahamika kama Fountain Gate.

Usajili wa Simba msimu huu unafanyika chini ya uangalizi wa tajiri mwenyewe, Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' aliyerejea katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live