Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yalimwa faini ya Mil. 1

Simba Yalimwa Faini Ya Mil. 1 Simba yalimwa faini ya Mil. 1

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi Kuu Tanzania TPLB katika kikao chake cha Machi 20, 2024 ilipitia mwenendo na amatukio mbalimbali ya Ligi na kufikia maamuzi kadhaa ikiwemo kuilima faini ya shilingi Mil. 1 Klabu ya Simba SC.

Simba imetozwa faini hiyo kwa kosa la mashabiki wake pamoja na walinzi wake wa uwanjani kupanga njama na kufanikisha azma ya kuingia uwanjani na kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina wakati mchezo dhidi ya Simba na Mashujaa FC ukiendelea kwenye Uwanja wa Azam- Complex, Chamazi jijini Dar Marchi 15, 2024.

Mashabiki hao walionekana kupitia video fupi iliyosambaa mitandaoni wakijadiliana na mlinzi wa uwanjani kabla hawajaingia uwanjani kufanya tukio hilo lililoleta taswira mbaya kwa Ligi na adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kuzingatia kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa klabu.

Mbali na hilo, walinzi wa uwanjani wa Simba, Kessy Mohamed, Mrisho Mindu pamoja na Mohamed Salmin na shabiki aliyefahamika kwa jina la la Mohamed Saleh, wamefungiwa kuingia viwanjani kwa kipindi cha miezi 12 kwa kosa la kushiriki katika tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live