Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yakwepa watekaji

16c0d15e54277b81e703cfc2c3e228d4.png Simba yakwepa watekaji

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Simba wamesafiri kwa ndege kuelekea mji mdogo wa Jos, Nigeria kuwakwepa watekaji.

Simba iko nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau FC ambayo makao makuu yake yapo Jos.

Kikosi hicho kilitua katika mji wa Abuja juzi na kilitaka kusafiri kwa basi kuelekea mji mdogo wa Jos kuwafuata wapinzani wao lakini Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk Benson Bana aliwatadharisha kutotumia usafiri huo kwani wanaweza kutekwa.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Simba jana walichapisha ujumbe kuwa walifanikiwa kupata ndege ya kwenda mji wa Jos, hivyo wamekwepa hatari ya kutekwa.

“Leo mchana (jana) kikosi kitakwenda kwa ndege mji wa Jos ambako ndio tutacheza mchezo dhidi ya Plateau FC, Jumapili kuanzia saa 12:00 jioni muda wa Tanzania,” alisema.

Wakiwa Abuja waliendelea kufanya maandalizi dhidi ya mchezo huo wakiwa na lengo la kushinda.

Wakimaliza kucheza mchezo huo watalazimika kurudi tena kwa ndege hadi Abuja kuun- ganisha ndege ya kurejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki moja baadaye.

Simba wakifanya vizuri mchezo wa ugenini na nyumbani basi watakutana na mshindi kati ya CD Do Sol au FC Platnum katika hatua inayofuata.

Hata hivyo Gavana wa Jimbo la Jos, Simon Lalong, ameahidi zawadi ya Naira Milioni 1 sawa na Dola za Marekani 2,600 kwa kila mchezaji wa Plateau United endapo wataifunga Simba.

Pia ameiahidi zawadi ya basi lenye siti 32 ambalo litakuwa mali ya klabu hiyo ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani.

Chanzo: habarileo.co.tz