Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yakwepa adhabu nzito TFF

Simba Yanga Kim Simba yakwepa adhabu nzito TFF

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba haitaadhibiwa na Bodi ya Ligi kwa wachezaji wake kuonyeshwa kadi tano za njano kwenye Dabi ya Kariakoo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Sheria, Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura. Adhabu itatolewa iwapo timu itapata zaidi ya kadi tano za njano.

Katika mchezo wa leo Jumapili, Oktoba 23 2022, Derby ya Kariakoo, klabu ya Simba SC imepata kadi za njano tano huku watani wao wa jadi, klabu ya Yanga SC ikipata kadi za Njano nne (4).

Mwamuzi wa mchezo, Ramadhani Kayoko ametoa kadi za njano 9 kama ifuatavyo;

Okra Augustine (Simba)

Feisal Salum (Yanga)

Mzamiru Yassin (Simba)

Mohamed Hussein (Simba)

Khalid Aucho (Yanga)

Tuisila Kisinda Aziz Ki (Yanga)

Djuma Shabani (Yanga)

Habib Kyombo (Simba).

Mpaka kipenga cha mwisho, timu zote zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1. Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Augustine Okrah dakika 15 kabla ya Aziz Ki kuisawazishia Yanga kwa mkwaju wa adhabu dakika ya 45 ya mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live