Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yakomba Sh bilioni 2.8

Simba Simba Simba.jpeg Simba yakomba Sh bilioni 2.8

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba msimu huu imejihakikishia kiasi cha Tsh 2.8 Bilioni kwa hatua ambayo imefikia ikivuna fedha nyingi kutoka kwa CAF baada ya timu hiyo kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa ikichukua kiasi cha Tsh 2.3 Bilioni.

Wekundu hao pia wamevuna Tsh 250 milioni kwa kushika nafasi ya tatu kwenye ligi, fedha ambazo zinatolewa kutoka Azam Media kupitia mkataba wa haki za matangazo ya Televisheni kwenye ligi.

Simba imevuna pia kiasi cha Tsh 50 kwa kuchukua ubingwa wa Muungano huku wadhamini wao Mbet ikiwapa jumla ya kiasi cha Tsh 150 kwa kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Tsh 50 milioni wakati ilipotinga robo fainali ikawapa tena Tsh 100 milioni na kuwafanya wekundu hao kuvuna jumla ya Tsh 2.8 bilioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live