Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yajivunia uzoefu CAF

Simbasctanzania Kikosi cha Simba SC

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba SC umetamba kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya kuiwakilisha vema Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, Oktoba 15, mwaka huu.

Simba imeanzia hatua ya kwanza ya michuano hiyo ambapo mechi ya kwanza itachezwa nchini Botswana, kisha marudiano Dar, Oktoba 22, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, amesema: “Kama uongozi tunaendelea kufanya maandalizi ya kikosi chetu kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, ni jambo zuri kuwa tunauelekea mchezo huu tukiwa na ari ya ushindi baada ya kuifunga Dodoma Jiji kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara.

“Bahati nzuri kwetu ni kwamba wachezaji wetu wana uzoefu na mashindano haya, lakini ubora wa kikosi tulichonacho ni sababu tosha ya kufanya vizuri.”

Msimu uliopita, Simba iliishia robo fainali ya michuano hiyo, huku ikiwa ni mara ya pili kwa misimu ya karibuni baada ya kufanya hivyo msimu wa 2018/19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live