Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yajeruhiwa, Namungo safi

Cb53883a37b8605bd54545437693a02f.png Simba yajeruhiwa, Namungo safi

Thu, 24 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKATI Namungo ikipata ushindi wa bao 2-0 katika mchezo wake wa Kombe la Shirikisho Afrika, hali ni tofauti kwa Simba baada ya kupata kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika jana.

Namungo walipata ushindi huo dhidi ya El Hilal Obeid ya Sudan katika Uwanja wa Azam Complex, wakati walipoteza mchezo wao na FC Platinum kwenye Uwanja wa Michezo wa Taifa, Harare, Zimbabwe.

Mabao ya Namungo yalifungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 14 na Steven Sey dakika ya 31 na la wapinzani wa Simba lilifungwa na Perfect Chikwende dakika ya 17.

El Hilal Obeid ambayo ilifika robo fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka 2017 na kushiriki mashindano hayo mara nne mfululizo walipata wakati mgumu kwa Namungo ambao hawakuwadharau wakiwa wamejiandaa vema kuwakabili.

Simba ambayo iliwakosa John Bocco na Aishi Manula inahitaji kucheza kufa kupona kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya timu hiyo ya Zimbabwe unaotarajiwa kuchezwa kati ya Januari 5 au 6 mwakani katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na kushinda ili iweze kufuzu hatua ya makundi.

Pamoja na kufungwa jana, Simba ilicheza vizuri lakini wapinzani wao walitumia nafasi ya kuwahi kufunga bao kujilinda zaidi badala ya kushambulia.

Katika mchezo wa marudiano Simba italazimika kushinda mabao 2-0 au zaidi ili kufuzu robo fainali, lakini endapo itaondolewa itaangukia Kombe la Shirikisho Afrika.

AS Kigali ya Rwanda imepewa ushindi wa mabao 2-0 baada ya wachezaji wawili wa KCCA ya Uganda kukutwa na corona huko Kigali hivyo watalazimika kushinda zaidi ya mabao matatu katika mchezo wa marudiano ili kuendelea na hatua inayofuata.

KCCA ilisafiri na wachezaji 15 lakini wawili walikutwa na corona na kubaki 13 hivyo mchezo haukuchezwa kwa sababu walitakiwa kuwa na wachezaji 15.

Zamalek ya Misri imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Bingwa Afrika baada ya klabu Gazelle FC ya Chad kujiondoa kutokana na serikali ya nchi hiyo kuizuia kusafiri kwenda Misri kucheza.

Chanzo: habarileo.co.tz