Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaizidi ujanja Berkane Morocco

Simba Tizi 4 Simba yaizidi ujanja Berkane Morocco

Thu, 24 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMA viongozi wa timu ya Renaissance Sportive de Berkane ama kwa kifupi unaweza kuiita RS Berkane walikuwa wakiisubiri Simba katika Mji wa Berkane, watakuwa wamepigwa chenga ya mwili kwani wenzao wameamua kuweka kituo Casablanca.

Jana Jumatano, msafara wa kikosi cha Simba, ulitua nchini Morocco na kuweka kambi fupi kwenye Mji wa Casablanca, kabla ya kwenda Berkane.

Awali ilielezwa timu hiyo ingeenda moja kwa moja kwenye mji wa Berkane ambako mchezo wa tatu wa Kundi D kunako Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utachezwa, lakini haikuwa hivyo.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa El Massira uliopo Berkane, saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezinyaka, kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, msafara huo jana asubuhi ulianza safari kuelekea Morocco ukitokea Istanbul, Uturuki tayari kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo.

Mtoa taarifa huyo alisema mara baada ya kutua Morocco, wataweka kambi fupi ya siku tatu kwenye mji wa Casbalanca kuanzia jana Jumatano hadi kesho Ijumaa ambapo wataelekea Berkane.

Aliongeza kuwa, lengo la kufika mapema Morocco ni kwa ajili ya kupata muda wa kutosha kupumzika na kuzoea hali ya hewa ili siku ya mchezo wasipate changamoto ya kimazingira kama ilivyokuwa Niger.

“Timu itafikia Casablanca na kuweka kambi fupi ya siku tatu kabla ya kwenda Barkane kuwakabili wapinzani wetu RS Barkane.

“Uongozi umeamua kupeleka timu Morocco mapema kwa lengo la kuwafanya wachezaji kupata muda wa kutosha wa kupumzika pamoja kuzoea hali ya hewa ili siku ya mchezo wasipate changamoto yoyote ya kimazingira.

“Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka za hali ya hewa inaeleza kuwa kwa sasa Morocco kuna baridi kali, hivyo tumeamua kwenda mapema kwa lengo la kuzoea mazingira.

“Tutakuwa Casablanca kwa siku chache kabla ya kuelekea huko Berkane ambako mchezo utachezwa hiyo Jumapili.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live