Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaizidi akili Wydad

Simba Sports Club Bunju Arena.jpeg Simba yaizidi akili Wydad

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Katika kuhakikisha Simba inapata matokeo bora dhidi ya Wydad tayari viongozi walishajipanga mapema huku Mwanaspoti likipenyezewa taarifa ya mratibu wa timu hiyo, Abbas Ally alishaweka mazingira salama ya kikosi hicho kitakapofikia kabla ya kutua.

Kwa upande wa kocha mkuu wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha alisema; “Katika mchezo uliopita tulikosa bahati tu ya kupata ushindi lakini wachezaji walipambana na kuonyesha ni kwa jinsi gani tulizihitaji pointi tatu, tunaenda ugenini kucheza na timu bora hivyo ni lazima tujipange ipasavyo.”

Wakati Simba ikizidi kujiimarisha kwa ajili ya mchezo huo, wapinzani wao tayari wameanza kuingiwa na mchecheto baada ya kubadilisha uwanja utakaotumika kutoka ule wa mwanzo wa Mohammed V uliopo jijini Casablanca na kuupeleka mechi Marrakech.

Simba inaingia katika mchezo huo ikihitaji kulipa kisasi kwani msimu uliopita iliondoshwa kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na Wydad baada ya kupoteza kwa mikwaju ya penalti 4-3.

Chanzo: Mwanaspoti