Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaitungua Geita kwa taabu 1-0, yamshusha Azam FC

Simba Full Time Simba yaitungua Geita kwa taabu 1-0, yamshusha Azam FC

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Geita FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Goli hilo pekee la Mnyama lilifungwa dakika ya 81 ya mchezo na kiungo wao mkabaji Babacar Sarr.

Simba sasa imefikisha alama 33 kwenye msimamo, chini ya Yanga anayeongoza akiwa na alama 40.

Simba ana kiporo kimoja kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza alingane na Yanga ambaye tayari ameshamaliza mzunguko wa kwanza kwa kucheza michezo 15.

Kwa ushindi huo, Simba amemshusha Azam FC ambaye ana alama 32 akiwa amecheza micheo 14.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live