Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaitafutia Azam mechi mbili

78862 Pic+simba

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benchi la ufundi la Simba limethibitisha kutafuta mechi mbili za kirafiki kabla la kukutana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Oktoba 23 kwenye Uwanja wa Uhuru.

Hilo limethibitishwa na Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems alisema wanahitaji mechi hizo kujiweka sawa.

Aussems amesema kwasasa wanaendelea na ratiba ya mazoezi huku wakisubiri uamuzi kutoka ofisi ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo Senzo Mazingisa.

Aussems amefafanua kuwa katika maombi yao wameomba kupatiwa mechi mbili ambapo kila wiki watakuwa wakicheza mechi moja.

Amesema bado hajapata majibu kutoka kwa Mazingisa juu ya ratiba kamili ya mechi hizo kama zitakuwa zimeshapatikana.

Simba inatajwa kujiandaa na ziara ya kwenda Mkoani Kigoma kucheza mechi mbili na klabu moja ya hapo huku pia mabingwa wa Burundi, Aigle Noir.

Pia Soma

Advertisement
Mbali na timu hizo pia klabu ya Bandari ya Kenya inatajwa kuwa katika mpango wa kuja nchini kucheza na Simba katika ziara yao ya mechi za kirafiki ikawemo Coastal Union.

Chanzo: mwananchi.co.tz