Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaisubiri Prisons Mbeya

4eea08fa8987a2855675e7a1ffe9f876 Simba yaisubiri Prisons Mbeya

Tue, 20 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba jana kilitua salama jijini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kukwaana na Tanzania Prisons keshokutwa mjini Sumbawanga.

Simba iliyopo katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16, kiko Mbeya ambako kitakaa kwa siku mbili kabla ya kwenda Sumbawanga, Rukwa, ambako wachezaji na Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sven Vandebrock alisema jana kuwa watapiga kambi Mbeya kwa siku chache kabla ya kwenda Sumbawanga, ambako watacheza na wapinzani wao hao.

Kocha huyo alisema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu, kwani Tanzania Prisons inatumia sana nguvu, lakini wamejipanga kuhakikisha wanashinda na kuondoka na pointi zote tatu ili kuzidi kujiweja pazuri.

Alisema kuwa kikosi chake kimeenda Mbeya kwa ndege kikiwa na wachezaji 22 huku kikiwa na matarajio makubwa ya kufanya vizuri.

Alisema wanaujua Uwanja wa Nelson Mandela, kwani walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA Cup) dhidi ya Namungo FC na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutwaa taji, hivyo hawatakuwa wageni na uwanja huo.

Wakati Simba wako Mbeya, wenyeji wao jana walikuwa wakikabiliana na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Simba wamejikusanyia pointi 13 baada ya kushuka dimbani mara tano, huku Azam ikiongoza baada ya kushinda mechi zao zote sita za awali na kujikusanyia jumla ya pointi 18 hadi sasa.

Yanga wenyewe nao wana pointi 13 sawa na Simba, baada ya kucheza mechi tano, lakini wako nafasi ya tatu baada ya kupitwa na wapinzani hao wa jadi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Yanga wenyewe keshokutwa watacheza dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa ligi tangu kuwasili kwa kocha wao mpya Cidric Kaze wakisaka pointi tatu muhimu katika mbio.

Chanzo: habarileo.co.tz