Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaipiga bao Newcastle

FoES98nXoAYPZXB Wachezaji wa Timu ya Simba SC

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya IFFHS kutoa orodha ya Ligi Bora duniani huku Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa nafasi ya 39 duniani na ya tano (5) Afrika, kuna orodha pia ya klabu 502 bora duniani.

Kwa mujibu wa IFFHS wameangalia matokeo ya klabu na mafanikio iliyoyapata kwenye kipindi cha kati ya Januari hadi Disemba 31, 2022.

Kwa hiyo kwenye kila nchi wamepima matokeo na mafanikio ya kila timu halafu wanalinganisha na timu nyingine ili kupata orodha ya nafasi ya timu ya kwanza hadi mwisho.

Kwenye tatu (3) bora ya klabu bora duniani, nafasi ya kwanza na ya pili zipo klabu za Brazil ambazo ni Flamengo na Palmeiras halafu nafasi ya tatu ipo Liverpool ya England. Klabu nyingine kubwa duniani hazipo kwenye tatu bora!

Al Ahly ya Misri imeshika nafasi ya 17 kwenye orodha hiyo, kwa maana hiyo Al Ahly ni bora kwenye takwimu kuliko klabu kama Barcelona, Napoli, AS Roma, Arsenal n.k.

Klabu ya Wydad Casablanca ipo nafasi ya 49 kwa ubora duniani na nafasi ya pili kwa Afrika. Wydad imezizidi klabu kama Atletico Madrid, Manchester United, Tottenham Hotspurs zote za Ulaya.

Kwenye orodha hiyo, klabu ya Simba ipo nafasi ya 107 Simba ipo juu ya klabu kama Mamelodi Sundowns, Raja Casablanca, Newcastle United, Valencia, Royal Antwerp.

Wananchi Yanga SC wenyewe wapo nafasi ya 199 juu ya klabu kama TP Mazembe, KRC Genk, New York City, Brighton & Hove Albion.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live