Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yailalamikia CAF waamuzi mechi yao na TP Mazembe kubadilishwa

51144 Pic+mwamuzi

Mon, 8 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kikosi cha Simba kikiendelea na maandalizi ya kujifua kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya TP Mazembe itakayochezwa Lubumbashi DR Congo uongozi wa timu hiyo ulipokea taarifa ya ghafla na kushtushwa.

Uongozi wa Simba umepokea taarifa hiyo kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa wamebadilisha waamuzi waliopangwa hapo awali kuchezesha mchezo wa marudiano kati ya TP Mazembe na Simba utakaochezwa Aprili 13.

Awali CAF ulitangaza waamuzi wa mechi ya kwanza kati yao ambayo ilichezwa hapa Dar es Salaam Aprili 6, na wengine ambao watachezesha mchezo wa marudianio.

Waamuzi wa awali waliopangwa na CAF, kuchezesha mchezo wa marudiano TP Mazembe na Simba ni Bamlak Tessema mwamuzi wa kati kutoka Ethiopia, Temesgin Samuel msaidizi namba moja kutoka Ethiopia, Gilbert Kipkoech Cheruiyot msaidizi namba mbili kutoka Kenya.

Wengine ambao walipangwa awali na CAF, mwamuzi wa akiba Peter Waweru kutoka Kenya.

Katika barua ambayo ilionyesha inatoka CAF, ambayo uongozi wa Simba uliipokea Aprili 7, ilisema kuwa waamuzi hao walibadilishwa kwa sababu ya kiiufundi ingawa hawakuziweka wazi.

Related Content

Baada ya CAF kufanya mabadiliko waamuzi wapya waliopangwa Janny Sikazwe kutoka Zambia atayekuwa mwamuzi wa kati, Berhe Tesfagiorgis kutokea Eritrea atakuwa msaidizi namba moja, Romeo Kasengele kutokea Zambia atakuwa msaidizi namba mbili, Audrick Nkole kutokea Zambia atakuwa mwamuzi wa akiba.

Wakati Aimable Habimana kutokea Burundi atakuwa Kamishna, Salah Ahmed kutokea Sudan atakuwa msimamizi wa waamuzi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori alisema wanafahamu miongoni mwa wamiliki wa timu hiyo Moise Katumbi shughuli zake nyingi huwa anafanya nchi Zambia ambapo waamuzi wa wapya waliopangwa kuchezesha mchezo huo wanatoka nchini humu.

Magori alisema awali walishapangwa waamuzi wa kuchezesha mechi zote mbili inakuaje baada ya mchezo wa kwanza umeshachezwa na matokeo yake kufahamika ndio wabadili waamuzi waliopangwa kuchezesha mechi ya marudiano.

Alisema tumeandika barua CAF, kuwalalamikia kuwa hatujalisishwa na jambo hili na atukubali kabisa kwa hali ya kawaida jambo hilo la kubadili waamuzi na kulinganisha ukubwa wa mechi na matokeo ya kwanza yalivyokuwa lazima timu yoyote itakuwa na mashaka.

"Kwa hali ya kawaida ukaribu wa Ndola Mji ambao atanoka mwamuzi mpya Sikazwe ambaye amepangwa kuchezesha mchezo wetu anatumia saa mbili tu kwa gari mpaka kuingia Lubumbashi DR Congo ambapo tutacheza mechi ya marudiano.

"Ukaribu huu wa waamuzi wapya kiukweli uongozi wa Simba umefikisha malalamiko CAF, ili kuweza kulishuhurikia jambo hili kabla ya mchezo wetu wa marudiano," alisema Magori.



Chanzo: mwananchi.co.tz