Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaigeukia Ihefu Ligi Kuu

D8d7b034a07bc7b6cceeb5451d176e80 Simba yaigeukia Ihefu Ligi Kuu

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SIMBA imedhamiria kutoa burudani kwa mashabiki wake na kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ihefu FC utakaochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo.

Simba ambayo ni bingwa mtetezi inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 32, inaingia kwenye mchezo huo ikitafuta ushindi kuendelea kupunguza tofauti ya pointi na Yanga inayoongoza kwa pointi 43. Ihefu inashika nafasi ya 17 ina pointi 13 inahitaji pointi tatu kurudisha morali kwani huo ni mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili.

Rekodi za mchezo wa raundi ya kwanza, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-1 uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Licha ya Simba kufanya vyema kwenye michezo minne iliyopita ya ligi, inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC.

Mwenendo wa mechi zake za mwisho za ligi kabla ya leo haukuwa mzuri kwani ilikuwa inapata ushindi mwembamba tofauti na ilivyozoeleka kwenye mechi za mwanzo za msimu kupata bao zaidi ya moja.

Ihefu mechi yake ya mwisho kwenye ligi ilifungwa mabao 3-0 na Yanga. Simba inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo kutokana na ubora wa safu ya ushambuliaji ikilinganishwa na wapinzani wao Ihefu ambayo mwenendo wake si wa kuridhisha.

Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck alisema wachezaji wameandaliwa vya kutosha kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

“Wachezaji wako tayari kwa mchezo, tunajua utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa tunakwenda kukutana na timu ambayo haina matokeo mazuri na wanatafuta ushindi,” alisema Sven.

Chanzo: habarileo.co.tz