Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaifuata Yanga kibabe yainyuka Azam mabao 3-2 Uwanja wa Taifa

97972 Pic+matokeo Simba yaifuata Yanga kibabe yainyuka Azam mabao 3-2 Uwanja wa Taifa

Thu, 5 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji Meddie Kagere aliingia akitokea benchi na kufunga bao la ushindi wakati Simba ikichapa Azam FC kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kagere alitumia dakika 10 tu baada ya kuingia kufunga bao hilo katika dakika 71, kutoka na uzembe wa mabeki wa Azam na kipa wao Razack Abarola walioshindwa kuokoa krosi ya Shomari Kapombe. Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Erasto Nyoni, Deo Kanda huku magoli ya Azam yakifungwa na Never Tigere na Idd Nado. Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 68 baada ya kucheza mechi 26, hivyo kuwafanya kuwa katika hali nzuri zaidi kabla ya kuwavaa watani zao wa jadi Yanga hapo Jumapili Machi 8. Katika mchezo huo wenyeji Azam walikuwa wa kwanza kupata bao dakika 5, lililofungwa na Tigere baada ya mabeki wa Simba kujichanganya katika kuokoa hatari golini kwao. Baada ya bao hilo Simba ilirudi mchezo na kuanza kumiliki mpira kwa pasi zao fupifupi na kufanikiwa kusawazisha bao katika dakika 9 kupitia Erasto Nyoni aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Luis Miquissone. Mkongwe Deo Kanda alifunga bao la pili kwa Simba akimalizia pasi mzuri ya Clatous Chama katika dakika 15. Simba baada ya kufunga bao la pili ilianza kucheza kwa mbwembwe kwa wachezaji wake kugongeana pasi fupifupi zilizoonekana kuwachanganya Azam. Simba waikuwa wanatumia zaidi upande wa Shomari Kapombe kupitisha mashambulizi yao ambao alikuwa anacheza sambamba na Deo Kanda na walionekana kufanikiwa. Azam walionekana kukosa utulivu hasa katika eneo la ushambuliaji ambalo alikuwa anacheza Obrey Chirwa na Shaban Chilunda lakini Chirwa alionekana kukosa msaidizi. Baada ya kuona hilo viungo wa Azam, Salum Abubakary na Bryson Rafael walikuwa wakitumia mipira mirefu kuweza kupenya ngome ya Simba, lakini Chirwa licha ya nguvu zake alikuwa akidhibitiwa. Azam ilirudi kwa kasi katika kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao katika dakika 49, lililofungwa na Nado aliyepiga shuti lililomshinda kipa Aishi Manula na kujaa wavuni. Baada ya Azam kusawazisha timu zote zilianza kucheza kwa umakini zaidi katika eneo la kati ya uwanja wakionekana kama wameridhika na matokeo. Kocha wa Simba, Sven alimtoa Kanda na kumwingiza Kagere mabadiliko yaliyokuwa na faida kwa vinara hao wa Ligi Kuu kwani mfungaji huyo bora wa msimu uliopita alitumia nafasi moja tu kuiadhibu Azam. Kagere alifunga bao akiunganisha vizuri krosi ya Kapombe ambayo beki wa Azam, Yakub Mohamed aliteleza huku kipa wake Abarola akiwa amechutama na kushindwa kuokoa mpira uliopigwa na Mnyarwanda huyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz