Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaichakaza Zimamoto yatinga nusu fainali Zanzibar

91129 Pic+simba Simba yaichakaza Zimamoto yatinga nusu fainali Zanzibar

Wed, 8 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba imemkaribisha kiungo wake mpya Luis Miquissone kwa ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Zimamoto kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba. Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na nahodha John Bocco, Sharaf Shiboub na Ibrahimu Ajibu huku lile la kufutia machozi la Zimamoto likifungwa na Hamad Hamad. Ushindi huo unaifanya Simba kufuzu kwa nusu fainali na sasa itacheza dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam Fc Januari 9, Huku Mtibwa wakisubili mshindi kati ya Yanga dhidi ya Jamhuri FC. Katika mchezo huo kocha wa Simba, Sven alimuingiza kiungo wake mpya aliyesajiliwa kutoka UD Songo, Luis Miquissone aliyeingia dakika 77, kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga. Wakati Miquissone akiingia tayari Simba ilikuwa mbele kwa mabao 3-1 katika mchezo huo ambao vijana hao wa Msimbazi walishindwa kuonyesha soka la kuvutia. Kiungo Ajibu alionyesha uwezo wake kwa kutengeneza bao la kwanza katika dakika 4 kwa pasi yake kumkuta, Bocco aliyeunganisha moja kwa moja mpira wavuni. Simba ilipata bao la pili dakika 8, lililofungwa na Shiboub akiunganisha kona ya Ajib ambayo iliongezewa nguvu na Erasto Nyoni na kumgonga beki wa Zimamoto na mpira ukakutana na Shiboub aliyefyatuka shuti kali na mpira kwenda wavuni. Simba ilitawala katikati kupitia kwa viungo wake Said Ndemla na Shiboub walikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kupiga pasi za uhakika. Dakika 12, Zimamoto walifanya shambulizi baada ya Ally Salim kupiga shuti kali lililodakwa na kipa Ally Salim aliyeidakia Simba kwa mara ya kwanza. Licha ya kufungwa mabao hayo Zimamoto ilionyekana kutokukata tamaa badala yake waliamua kucheza mpira na kuwapa wakati mgumu klabu ya Simba. Zimamoto walikuwa wakitumia njia ya kupiga mashuti ya mbali kupitia kwa kiungo wao Ally Salim, lakini alikuwa akikutana na changamoto ya umakini kwa kipa Ally Salim wa Simba. Zimamoto ilipata bao kupitia kwa Hamad Hamad ambaye alizidiana nguvu na beki wa Simba, Erasto Nyoni na kumfanya apige shuti dogo lililoenda moja kwa moja wavuni. Katika kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi na kuonyesha wanahitaji magoli mengi zaidi na dakika 53 kiungo Shiboub alipiga pasi mpenyezo kwa Ibrahim Ajibu ambaye alipiga mpira kwa kuuzungusha na kwenda moja kwa moja wavuni.

Chanzo: mwananchi.co.tz