Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaibamiza Ihefu

4942a6a13f3c0567beb49d3168243c1e.png Simba yaibamiza Ihefu

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SIMBA imeendelea kuwapa burudani mashabiki wake baada ya kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Ihefu FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam jana.

Katika mchezo huo, ushindi wa Simba uling’arishwa kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Meddie Kagere aliyefunga mawili dakika ya 15 na 40 akitumia vema pasi zilizopigwa na Clatous Chama na Said Ndemla, na Mohamed Hussein ‘T Shabalala’ alifunga dakika ya tisa akimalizia pasi ya Shomari Kapombe, huku Chris Mugalu akimalizia bao la nne dakika ya 83.

Huo ni ushindi mkubwa kwa Simba tangu walipoibuka na mabao 7-0 dhidi ya Coastal Union mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Novemba 21, 2020.

Matokeo hayo yamewafanya Simba kufikisha pointi 35 wakiendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo nyuma ya kinara Yanga wenye pointi 43, wanaotarajia kucheza leo dhidi ya Tanzania Prisons. Huku Ihefu FC wakisalia nafasi ya 17 na pointi zao 13 baada ya kucheza michezo 18.

Kipindi cha pili kilianza kwa kufanya mabadiliko ya wachezaji, timu zilianza kucheza mpira wa wazi na kushambuliana kwa zamu na Ihefu ilifanikiwa ku. Katika mchezo wa raundi ya kwanza timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Simba ilishinda 2-1 kwa mabao ya John Bocco na Mzamiru Yassin wakati lile la Ihefu likipachikwa na Omary Mponda.

Kadri muda ulivyozidi kwenda timu hizo zilionekana kujuana kwa maana ya kimbinu lakini hata hivyo Simba waliokana kubadilisha mbinu na kutumia uzoefu kila walipokuwa wanavuna mstari wa kati walikuwa wanashambulia kwa kupiga pasi ndefu.

Ushindi huo unaiweka Simba katika nafasi nzuri ya kupambana na FC Platinum ya Zimbabwe wiki ijayo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika. Katika mchezo wa kwanza, Simba walifungwa 1-0.

Chanzo: habarileo.co.tz