Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaibadilishia mbinu Tanzania Prisons

Simba Final Dir Simba yaibadilishia mbinu Tanzania Prisons

Wed, 14 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba leo Jumatano kitakuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha kuwa kinaibuka na ushindi mbele ya Tanzania Prisons ambapo kuelekea katika mchezo huo Kocha Juma Mgunda ameweka wazi kuhitaji nguvu ya ziada ili kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Simba iacheza na Prisons katika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ambapo wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya KMC.

Kocha Mgunda alisema kuwa kuelekea katika mchezo huo wanayo kazi kubwa ya kufa nya kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi mara baada ya kutoka sare katika mchezo uliopita wa ligi na ubora wa timu hiyo wanapiokuwa katika uwanja wao wa nyumbani.

“Tunahitaji nguvu ya ziada kuhakikisha kuwa tunaibuka na ushindi katika mchezo wetu wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambapo timu hii huwa bora zaidi haswa linapokuja suala la wao wanacheza wakiwa nyumbani kwao.

“Kikubwa kwetu ni kuhakikisha kuwa tunapata matokeo, tayari kama timu tunaamini kuwa kuna morali nzuri haswa baada ya kufanikiwa kushinda ugenini katika mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika hivyo tutaoa kilicho bora kwa ajili ya faida ya timu,” alisema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live