Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yahamisha makali ya Caf Ligi Kuu Bara

Usajili Simba SC Simba yahamisha makali ya Caf Ligi Kuu Bara

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KATIKA kuhakikisha wanautetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba wametamba kurejesha makali yao ya Kombe la Shirikisho Afrika katika Ligi Kuu Bara.

Hiyo ikiwa ni siku imepita tangu Yanga itoke kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba ambayo jana ilitarajiwa kujitupa uwanjani kuvaana na Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast, hivi ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 37 huku Yanga wakiongoza wakikusanya 48.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa licha ya wapinzani wao kuongoza katika msimamo wa ligi, lakini bado wana nafasi ya kubeba taji hilo.

Ally alisema kuwa kasi wanayoendelea nayo katika Shirikisho ya kufanya vizuri iliyowafanya wakae kileleni katika Kundi D (kabla ya mchezo wa jana), ndiyo watakayorudi nayo mara watakaporejea kwenye ligi.

Aliongeza kuwa jeuri hiyo wanaipata baada ya kurejea kwa wachezaji wao wenye majeraha ambao ni Chris Mugalu, Kibu Denis na John Bocco.

“Tuliowabakisha nyumbani wakati sisi tukiwa katika Shirikisho, tunawakumbusha waache kuzurura hovyo, waache kujifanya wafugaji wafanye mazoezi kweli.

“Na kama wana mechi washinde, kwani Simba akirejea kutoka Benin, moja kwa moja tutarejea kwenye ligi na hapo ndipo watatutambua ule moto ambao tumeuwasha Caf.

“Tulichopanga ni kurejesha yale makali tunayoyafanya katika Shirikisho kuyahamishia katika ligi, tunaamini kiwango cha kila mchezaji wetu, hivyo Wanasimba waondoe hofu,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live