Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yahaha kibali cha Lwanga

E5554aababeb9058a7a4f3fed886dc1c Simba yahaha kibali cha Lwanga

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KIUNGO mpya wa Simba, Taddeo Lwanga huenda akashindwa kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa michezo wa Taifa, Harare, Zimbabwe kesho.

Lwanga amesajiliwa akiwa mchezaji huru kipindi hiki cha dirisha dogo kuziba nafasi ya Gerson Fraga anayeuguza tatizo la goti alililolipa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United. Akizungumza kupitia mtandano wa Youtube kutoka Zimbabwe jana, Mtendaji Mkuu Simba, Barbara Gonzalez alisema bado wanaendelea kupambana kuhakikisha wanapata kibali cha mchezaji huyo ili aweze kucheza mchezo huo.

“Bado tunaendelea kupambana kupata kibali ili acheze ndani ya wakati na mategemeo yetu kuanzia leo (jana) au kesho (leo) tutakipata,” alisema

Barbara alisema Lwanga yupo Harare na Simba na anaendelea na mazoezi na wenzake kujiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji FC Platnum na wapo kwenye hatua za mwisho kwani wamewasiliana na klabu yake ya zamani ya Tanta FC ya Misri.

Pia alisema wachezaji wengine wanaendelea vyema na wanafanya mazoezi kwani dhamira yao ni kufanya vyema kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa. Barbara alisema mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 9:00 alasiri kwa saa za Zimbabwe ambapo kwa Tanzania itakuwa saa 10:00 jioni na kuwaomba mashabiki kuzidi kuwaombea washinde.

Baada ya mchezo huo Simba itarejea nyumbani kujiandaa na mchezo wa marudiano uliopangwa kuchezwa kati ya Januari 5 au 6 mwakani. Endapo Simba itaitoa timu hiyo itafuzu robo fainali, lakini ikiondolewa itaangukia Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: habarileo.co.tz