Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yagaragazwa na Raja kwa Mkapa, waburuza mkia kundi C

Simba Wapigwa 3 Simba imekubali kichapo cha mabao 3-0

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Klabu ya Simba wamechezeakipigo kitakatifu cha mabao 3-0 kutoka kwa Raja Casablanca ya Morocco.

Mchezo huo wa hatua ya Makundi umewashuhudia Simba kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003 wakipoteza mchezo uwanja wa nyumbani kwa mara ya kwanza hatua ya Makundi.

Simba waliokuwa na rekodi bora katika Uwanja wa nyumbani leo walijikuta katika wakati mgumu licha ya kucheza mpira kwa muda mrefu.

Magoli ya Raja Casablanca yamefungwa na H. Khabba 30', S. Benjdida 83' na I. Mokadem kwa mkwaju wa penati iliyosababishwa na beki Joash Onyango.

Kwa matokeo hayo Raja wanapanda mpaka nafasi ya kwanza kundi C wakiwa na alama zao 6, wakifuatiwa na Horoya wenye alama 4, Vipers wakiwa na alama 1 huku Simba wakiburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live