Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafungukia ishu ya Saido

Saido 38834065 Simba yafungukia ishu ya Saido

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati akiwa ni mchezaji wa pili kukutana na Thank You ndani ya Simba, mwamba Saido Ntibanzokiza uongozi wa timu hiyo umefungukia uwezo wake.

Ntibanzokiza Juni 18 aliagwa rasmi na Simba hivyo hatakuwa ndani ya kikosi hicho msimu wa 2024/25 akiungana na nahodha John Bocco.

Ipo wazi kuwa Ntibanzokiza ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Simba msimu wa 2023/24 akitupia mabao 11 ni saba alitupia kwa mikwaju ya penalti.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa mchezaji huyo alikuwa anaipenda kazi yake kila wakati na alikuwa anatoa ushirikiano mzuri.

“Saido Ntibanzokiza hatutakuwa naye msimu ujao ni moja ya wachezaji waliokuwa wakifanya kazi kwa kujituma na anapenda kazi yake hivyo tunamtakia kila la kheri.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live