Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafunguka kinachomsumbua Okrah

AHMED NA OKRAH Simba yafunguka kinachomsumbua Okrah

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ukimya wa muda kupita, hatimaye uongozi wa Simba SC umeweka wazi kuwa kiungo wao mshambuliaji wao Augustine Okrah, alivunjika kidole kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ametoa maelezo hayo mapema hii leo Marchi 13, 2023, alipokuwa akizungumzia maandalizi ya mechi yao dhidi ya Horoya mechi itakayopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Tunamshukuru Mungu wachezaji wetu waliocheza mechi dhidi ya Mtibwa hakuna hata mmoja aliyepata majeraha, majeruhi tulionao ni wale wale wachache kama Augustine Okrah ambaye alivunika kidole kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Al Hilal, ameanza mazoezi lakini bado hajaanza kupiga mpira," alisema Ahmed.

Ahmed alimtaja majeruhi mwingine ambaye bado anajiuguza ni Ismail Sawadogo huku Kibu Denis akirejea kikosini baada ya kukosa mechi mbili za Simba dhidi ya Vipers SC ya marudiano na moja ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live