Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafunguka aliko Kibu na Chama

Kibu, Chama Edqq Simba yafunguka aliko Kibu na Chama

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wachezaji wao, Clatous Chama, Luyis Miquissone na Kibu Denis bado ni majeruhi na watakaa nje kwa muda wakijiuguza kabla ya kurejea tena dimbani.

Ahmed amesema hayo mara baada ya Simba kuichapa Azam FC mabao 3-0 mchezo wao wa Ligi uliopigwa jana katika Dimba la Mkapa na kuongeza kuwa, Simba sasa imeimarika na kurejesha makali yake.

“Chama ni majeruhi, aliumia kwenye nusu fainali ya kombe la Muungano, aliumia nyama za paja, hata Miquissone naye aliumia nyama za paja kwa hiyo bado wanaendelea na matibabu. Kwa mujibu wa taarifa za daktari wanahitaji siku kama 8 hivi ili waweze kupona sawasawa.

“Kwa upande wa Kibu Denis aliumia enka kwenye mchezo dhidi ya Namungo, kwa hiyo na yeye anahitaji muda ili aweze kupona sawasawa, lakini vijana wetu wote wanaendelea na matibabu na wakikaa sawasawa watarejea kuja kuitumikia Simba katika mechi za mwisho wa ligi” amesema Ahmed Ally.

Katika msimamo wa Ligi, Yanga wanaongoza wakiwa na alama 68 katika michezo 25, Azam nafasi ya pili alama 57 na michezo 26 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 56.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live