Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafanya umafia CAF

Fb XAFuXoAUTdZS Simba yafanya umafia CAF

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Simba wako Dar es Salaam kimwili lakini akili na mipango yao yote ipo Lilongwe Malawi.

Katika kuhakikisha wanaanza kwa umakini kabisa kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets jana Jumanne kuna msafara wa watu maalumu watatangulia Malawi kwa ajili ya kuweka mazingira sawa.

Msafara huo wa watu maalumu utakwenda kuhakikisha mazingira na vitu muhimu vya ndani ya nje ya uwanja kabla ya timu kufika Alhamisi vinakuwa kwenye mpangilio mzuri na kuepuka fedheha yoyote kutoka kwa wageni ambao wameahirishiwa mechi zao mbili za Ligi ili kujiandaa kikamilifu.

Simba itacheza mechi ya kwanza ya hatua ya awali ugenini Jumamosi ya Septemba 10 kabla ya kurudiana nao Uwanja wa Benjamin Mkapa maarufu kama machinjioni Septemba 17.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz