Mon, 29 May 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Wakati wengi wakijiuliza alipo mlinda mlango wa Simba aishi Manula na wakati huo huo tetesi zikizagaa kuwa anaondoka kwenda kujiunga na Azam FC.
Hatimaye Klabu ya Simba kupitia kwa Meneja wake wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally wameweka wazi alipo Mchezaji huyo.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Ahmed ameandika;
"Kipa wa Taifa Aish Salum Manula yupo Nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya nyama za paja"
Mungu amjaaalie nyanda wetu matibabu yake yaende vizuri"
Manula amekosekana katika mechi kadhaa za Simba hali iliyozua wasiwasi kwa Mashabiki wengi wa Simba SC.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: