Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaelekeza nguvu Ligi Kuu

Pablo Martin Francoi Pablo Franco , Kocha mpya wa Simba SC

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Wekundu wa Msimbazi, Pablo Franco, amesema baada ya timu kurejea kutoka kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika na wachezaji kupewa mapumziko ya siku moja, sasa wanaelekeza nguvu na akili katika mchezo wao wa Ligi Kuu NBC.

Pablo ameweka wazi kuwa wana michezo miwili ya Ligi inayofuatana ambayo ni dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji kabla ya kurudiana na RS Berkane katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha wanashinda michezo yote.

"Biashara ni Timu nzuri inacheza kitimu pia ina wachezaji wazuri mmoja mmoja. Inapocheza na timu kubwa inatoa upinzani mkubwa lakini tutahakikisha tunapambana kupata ushindi jambo zuri ni kuwa tupo nyumbani tena mbele ya mashabiuki wetu" amesema Pablo

Kwa upande wake nahodha John Bocco akili za wachezaji wamezihamishia katika mechi hizo mbili za Ligi kwanza kabla ya kukutana na Berkane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live