Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yabanwa mbavu na Namungo, yadondosha pointi

Simbasctanzania 279601552 1012844172990354 1646444986738024666 N 1 Simba yabanwa mbavu na Namungo, yadondosha pointi

Tue, 3 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Soka ya Simba imeambulia sare katika pambano lake la Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo kwenye Uwanja wa Ilulu.

Klabu ya Namungo ilianza kwa kupata bao kupitia kwa mchezaji wake Jacob Masawe katika dakika ya 8 kabla ya Shomari Kapombe kusawazisha mnamo dakika ya 42 na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa na matokeo ya sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa Namungo kupata bao la utangulizi kupitia kwa mshambuliaji wake Obrey Chirwa dakika ya 54 kabla ya Kibu Denis Kuchomoa mnamo dakika ya 79 na kusababisha pambano kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 2-2.

Kwa matokeo hayo Simba inabaki katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi ikiwa na jumla ya alama 43 ikiwa tayari imecheza michezo 21 huku kinara akiwa ni Yanga mwenye jumla ya alama 55 akiwa tayari naye amecheza michezo 21, klabu ya Namungo wao wanasalia kwenye nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya alama 29.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live