Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yabakiza alama saba kuikamata Yanga kileleni

GIfRlnBWgAEn0IU.jpeg Simba yabakiza alama saba kuikamata Yanga kileleni

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ushindi wa mabao 3-1 ambao Simba imeupata usiku wa jana, Jumanne kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi dhidi ya Singida Fountain Gate umeifanya kupunguza tofauti ya pointi kati yake na Yanga kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara kubaki saba.

Awali, Yanga ambao walikuwa mbele kwa mchezo mmoja, walikuwa wakiongoza msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 10 baada ya kuichapa Ihefu SC jana Junatatu, mvua ya mabao 5-0 kwenye uwanja huo uliopo Dar es Salaam.

Mabao ya Simba kwenye mchezo wa jana yamefungwa na Sadio Ntibazonkiza katika dakika ya tano na tisa (amefikisha mabao saba) huku chuma ya tatu ikifungwa na Freddy Koublan dakika ya 34 huku la Singida FG likifungwna Thomas Ulimwengu dakika ya 84.

Simba ilizianza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikiwa na uchu wa kusaka mabao kutona na safu yake ya ushambuliaji kufika mara nyingine kwenye eneo la Singida FG.

Clatous Chama na Sadio ndio wachezaji ambao walionekana kuwa na madhara zaidi kwa Singida FG ambao walionekana kutokuwa na nidhamu ya kutosha katika kujilinda jambo ambaloliliwafanya nyuma kuwa wazi.

Simba ilionekana kujenga mashambulizj yake hasa kutokea pembeni ambako mabeki wake wa pembeni, Israel Mwenda na Mohammed Hussein 'Tshablala' walikuwa wakiongeza namba.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Simba ilienda mapumzika ikiwa mbele kwa mabao 3-0, waliporejea kipindi cha pili walikuwa na kazi moja tu ya kulinda matokeo hayo.

Licha ya mabadilko kadhaa ambayo yalifanyika katika kipindi cha pili ikiwemo kutolewa kwa Mzamiru Yassin na Mwenda huku wakingia David Kameta na Shomary Kapombe Simba iliendelea kuwa imara lakini ilipoteza nguvu ya kushambulia tofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 42 na imeendelea kusalia katika nafasi ya tatu, wamezidiwa pointi ni mbili kati yao na Azam FC ambao wapo nafasi ya pili huku wakiwa mbele kwa michezo miwili.

Yanga ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 49 kileleni.

INONGA APUMZISHWA

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilitoshwa kwa beki Mkongomani, Henock Inonga kutokana na dhoruba ambazo alikumbana nazo kwenye mchezo huo.

Inonga ameshindwa kuedelea na dakika 45 za kipindi cha pili jambo ambalo liliwafanya Simba kuwa na mpango mbadala ambao ulikuwa ni kumuandaa Kennedy Juma wakati wa mapumzika ili kuchukua nafasi yake.

Baada ya mabadiliko hayo mara tu baada ya wachezaji kurejea kipindi cha pili, Inonga alionekana akirudi kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akichechemea.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: