Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaanza mipango kuisaka Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa

Simba Kuondoka Dar Kesho, Kumsubiri Prisons Morogoro.jpeg Simba yaanza mipango kuisaka Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema wameshaanza kusuka mikakati ya kufanya vizuri katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa lengo la kuhakikisha wanaondoa uteja wa kung'olewa kwenye hatua hiyo.

Ahmed amesema kwa misimu mitano mfululizo kuishia hatua hiyo inatosha na sasa wanataka kufika fainali, hivyo wakiwa wanasubiri ratiba ya kukutana na mpinzani gani tayari wameanza mikakati.

"Tumejifunza mengi kupitia hatua ya robo fainali baada ya kufanya hivyo kwa miaka mitano mfululizo sasa mikakati ya kuvuka hatua inayofuata imeanza," amesema Ahmed.

"Tumeingia katika orodha ya timu tano bora kuingia kwenye hatua ya robo fainali mara tano mfululizo sio jambo dogo inaonyesha ni namna gani viongozi wana mipango thabiti."

Amesema mpinzani yeyote watakayekutana naye watahakikisha wanapambana naye ili kuhakikisha kwamba wanavuka hatua hiyo na kuanza mikakati ya nusu fainali na hatimaye fainali.

"Mashabiki wetu tunawashukuru kwa ushirikiano na moyo wao wa kuendelea kuiunga mkono timu yetu kuanzia uongozi wa juu wanatoa shukrani zao," alisema.

Droo ya michuano hiyo kwa ajili ya robo fainali inatarajiwa kufanyika Machi 13, mwaka huu, huku Simba wakitarajiwa kukutana na kati ya Mamelodi Sundowns, Al Ahy au Petro Atletico.

Chanzo: Mwanaspoti