Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaanza maandalizi msimu wa 2021/22

Barbara Pic Data Simba yaanza maandalizi msimu wa 2021/22

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author Simba ni kama imepania kuanza vizuri msimu ujao baada ya kuanza kuingia sokoni mapema kusaka vifaa vipya na jezi mpya watakazotumia wachezaji.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez leo Desemba 17 ameweka picha katika mitandao yake ya kijamii akiwa katika moja ya duka la vifaa vya michezo nchini Afrika Kusini huku akiwa anachagua baadhi ya vifaa.

Katika picha hizo, Barbara ameunganisha na ujumbe wa maneno ambao ulionyesha kuwa Simba wameanza maandalizi ya msimu ujao.

"Tunajiandaa na msimu wa 2021/22 mapema. Jana nimezunguka Jo’berg kutafuta vifaa vipya kwa timu yetu kwa majadiliano na kocha, pia kupata chaguo na miundo ya jezi. Ukianza mapema, utapata kila unachokitaka,” ameandika Barbara.

Simba tayari imetambulisha jezi inazotumia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na watasafiri mwishoni mwa wiki hii kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa mtoano dhidi ya FC Platinum utakaopigwa Desemba 23 kabla ya kurudiana jijini Dar Januari 6.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz