Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaachiwa msala wa Morrison

Bm Pic 2 Data Simba yaachiwa msala wa Morrison

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author SIKU chache baada ya kuzagaa kwa video inayomuonyesha winga wa Simba, Bernard Morrison ‘BM3’ akionyesha ishara ya tusi, imewaibua mabosi wa Bodi ya Ligi (TPLB) na kuwaachia Wekundu wa Msimbazi msala wa Mghana huyo wakidai wao ndio wanaopaswa kumshughulikia kwanza.

Mpaka sasa sio viongozi wa Simba wala wasimamizi wa soka waliozungumzia suala hilo ambalo miaka michache iliyopita liliwahi kumponza nyota wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Athuman Idd ‘Chuji’ alipowaonyesha mashabiki kidole cha kati walipokuwa wakimzomea.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), Steven Mnguto alipoulizwa kulikoni juu ya ukimya kuhusiana na video na kitendo alichofanya winga huyo wa zamani wa Yanga, alisema kinapaswa kwanza kuchukuliwa hatua na viongozi wa timu yake kisha liende TFF.

Mnguto alisema hadi sasa hajaona wala kusikia hatua zozote zilizochukuliwa na Simba dhidi ya mchezaji huyo, lakini akadokeza kwa upande wao kama litafika mezani kwao watalipeleka katika kamati ya nidhamu ambayo ndio ina mamlaka ya kutoa uamuzi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz