Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ya kwanza kutua Liti, mashabiki wamshangilia Pluijm

Liti Simba SC Simba ya kwanza kutua Liti, mashabiki wamshangilia Pluijm

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba kimekuwa cha kwanza kuwasili katika uwanja wa Liti mkoani hapa.

Simba imewasilia saa 8:13 mchana ambapo nahodha Mohammed Hussein 'Tshabalala' alikuwa wa kwanza kuteremka katika gari.

Wa pili alikuwa kocha wa Simba Juma Mgunda ambaye mashabiki walimshangilia kwa nguvu.

Kikosi Cha Singida Big Stars kimetua uwanjani saa 8:22 huku kocha wa timu hiyo Hans Van Pluijm akishangiliwa na mashabiki.

SBS inatarajia kucheza saa 10 jioni dhidi ya Simba SC mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Mara baada ya kuingia uwanjani mchezaji wa kwanza kushuka katika basi alikuwa beki wa kushoto Shafiq Batambuzi na kisha kufuatiwa na Plujim

Mara baada ya kushuka Pluijm mashabiki walianza kumshangilia huku nae akipiga makofi.

Mchezaji mwingine aliyeshangiliwa na mashabiki ni Paul Godfrey 'Boxer'

Wachezaji hao waliingia katika vyumba vya kubadilisha nguo kabla ya kuanza kwa mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live