Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba ya Benchikha imeanza kuwa tamu

Benchikha Morocco.jpeg Simba ya Benchikha imeanza kuwa tamu

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ama hakika huyu ni kocha wa makombe na ni kocha mkubwa barani Afrika, Simba SC wamepata kocha kweli kweli jinsi ambavyo ukiangalia alivyoibadilisha timu ndani ya siku 10 tu tangu akabidhiwe timu hii.

Timu aliikuta haina morali ya kueleweka, timu ilikuwa haina shauku ya kutaka kufanya vizuri, timu haikuwa na muunganiko, timu ilikuwa na makundi makundi ya wachezaji pia baadhi ya viongozi.

Ameweza kuunganisha hizi changamoto zote ndani ya muda mfupi, na unaona Kwa Sasa timu inacheza vizuri Sana, timu inatengeneza nafasi za kutosha sema wafungaji ndio tatizo.

Timu inakaba kwa nidhamu, ina shambulia kwa nidhamu kubwa lakini kikubwa zaidi ni kuwa na morali na shauku ya kutaka kufanya vizuri Kwa wachezaji wote ambao walipata nafasi ya kucheza juzi.

Huyu ni mwalimu ambaye kama viongozi watamsikiliza na wakamsajilia wachezaji ambao anawataka basi Simba tutaishuhudia ikifika mbali hususani msimu ujao.

Juzi kila eneo lilikuwa Bora Sana, wachezaji walipambana Sana kutaka matokeo lakini mpira wakati mwingine una matokeo ya kikatili Sana.

Poleni mashabiki wa Simba SC, lakini bado nafasi ipo kubwa tu endapo Michezo ijayo timu ikipata matokeo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live