Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba watua kinyonge

Wametua Pic Data Simba watua kinyonge

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KUFUNGWA ni msiba, ukitaka kuthibitisha hilo, iulize klabu ya Simba baada ya kuchapwa na Kaizer Chiefs mabao 4-0 nchini Afrika Kusini na kutua nchini kinyonge.

Simba imerejea nchini leo Jumatatu ya Mei 17,mwaka 2021 baada ya kutua Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere walikuwa wamepoa kama vile wana msiba.

Hali halisi ilivyokuwa leo sio wachezaji, makocha wala viongozi sura zao hazikuwa na furaha tofauti na ilivyozoeleka wakishanda ambao wanakuwa na nyuso za bashasha,ambapo wanakuwa huru kuongea na Wanahabari.

Mastaa wa timu hiyo, waliokuwa wanapita mbele ya Wanahabari kwa kuuchuna, huku baadhi wakiwa wamevalia kofia aina ya kepu ambazo walizishusha hadi kwenye vipanda uso na walivaa na  barakoa, hivyo ikawa ngumu kutambulika kirahisi kwa baadhi yao.

Mwanaspoti lilipowafuata ili kuzungumza nao mawili,matatu kuhusiana mechi hiyo, hawakutoa ushirikiano baadhi yao wakiweka wazi kukatazwa kuzungumza chochote.

Hata mashabiki ambao wamezoea kuwaita na kutamani kupiga nao picha na waliogopa hata kuwasogelea kutokana na jinsi walivyoingia na sura za huzuni kama wamefiwa.

Kitendo hicho kimewafanya mashabiki kuwa na manung'uniko kuwaona hawawatendei haki wanapofungwa kama wanawatenga.

WACHEZAJI MAPUMZIKO Leo wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja, kesho wataanza mazoezi saa 10 katika Uwanja wao wa Mo Simba Arena uliopo Bunju, hiyo ni taarifa kutoka kwa meneja wa klabu hiyo,  Patrick Rweyemamu. Afisa habari wa timu hiyo, amezungumzia kwa ufupi kwamba licha ya kufungwa Simba ni klabu kubwa wanajipanga kwa mechi ya nyumbani. "Simba ni klabu kubwa, tunajiandaa kwa ajili ya mchezo wa tarehe 22 kesho tutaanza mazoezi ya moja kwa moja na tutakuwa na kesho tutakuwa na  mkutano na Wanahabari, kuzungumzia safari mzima," amesema.

Viongozi waliokuwepo pamoja na kikosi ni Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi na Mohamamed Nassorona Afisa Mtendaji mkuu wa zamani, Crescentius Magori.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz