Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba watua Dar, kuanza kuwawinda Coastal Union

Simba Warejea Simba watua Dar, kuanza kuwawinda Coastal Union

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, leo Januari 23, 2023, wamerejea jijini Dar na wachezaji kupewa mapumziko ya siku moja kabla ya kuanza mazoezi hapo kesho, Januari 24, 2023.

Kwa mujibu wa taarifa waliyoipost kwenye Simba App, wachezaji wote watarea kambini kesho kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Azam Sports Federation (ASFC) dhidi ya Coastal Union, Jumamosi hii Januari 28, 2023.

Mazoezi hayo yatafanyika katika Uwanja wa Mo Simba Arena ambapo Simba wanasema, wanataka kushinda kila mechi katika michuano hiyo ili waweze kushinda kila kikombe.

Simba walitokea Dodoma walipokipiga na Dodoma Jiji Januari 22, 2023 na kufanikiwa kuondoka na alama tatu baada ya ushindi wa goli 1-0 bao lililowekwa nyavuni na mshambuliji mpya wa kikosi hicho Jean Baleke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live