Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba watoa tamko suala la kusimamisha wachezaji

Ahmed Ally Semaji La Simba.jpeg Simba watoa tamko suala la kusimamisha wachezaji

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamefungukia ishu ya kuwasimamisha wachezaji iliyoibuka hapo jana Novemba 7, 2023 baada ya Simba kutangaza kuachana na Kocha Mkuu Roberto Oliviera 'Robertinho'.

Tetesi ziliibuka kuwa, Simba wamewasimamisha nyota kadhaa wakiwemo Clatous Chama, Henock Inonga na Shomari Kapombe ndipo Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally alipozungumzia ishu hiyo alipokuwa akielezea maandalizi ya mechi yao ijayo dhidi ya Namungo FC.

"Wanasimba wanatakiwa watulie, wawaache viongozi wafanye kazi yao watakuja na maamuzi sahihi katika wakati husika. Huwezi kusema sasa hivi unasimamisha sijui wachezaji kumi wakati tuna mechi zinakuja hivyo tunaomba mtuamini sisi viongozi," alisema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live