Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba watamba kufika kufika mbali Kimataifa

ROBERTINHO KUELEKEA MCHEZO WA KESHO Kocha wa Simba, Mbrazili Roberto Oliveira ‘Robertinho’

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema kikosi chake kipo tayari kuwakabili mabingwa wa Morocco, Wydad Casablanca.

“Tupo tayari kwa mchezo na ninaamini tutashinda, sababu wachezaji wangu wana ari kubwa ya kupambana. Najua utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora waliokuwa nao wapinzani wetu lakini tupo tayari kwa mapambano lengo ni kupata ushindi,” amesema Robertinho

“Tangu siku ya kwanza najiunga na Simba SC niliona kuwa tuna uwezo wa kufika mbali katika michuano hii hata fainali na hii ni kutokana na kikosi kusheheni wachezaji wenye uzoefu wa michuano mikubwa, lakini pia malengo yaliyowekwa na uongozi wa klabu hii,” amesema Robertinho

Chanzo: www.tanzaniaweb.live