Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba watakabidhiwa uwanja Jumamosi - Mtumbuka

KWA MKAPAAA Uwanja wa Mkapa

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba ikiwa na jambo lake huwa haina utani. Si mnajua kesho Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam itakuwa wenyeji wa Raja Casablanca kwa ajili ya mechi ya Kundi C ya Ligi ya Mabingwa Afrika? Sasa sikia hii.

Huku wanachama kadhaa wakionekana kurandaranda magetini, Meneja wa Uwanja wa Mkapa, Salum Mtumbuka amesema kuwa Simba itakabidhiwa Uwanja Jumamosi na si vinginevyo.

Aliongeza kuwa jukumu la kuulinda uwanja huo ni Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT ndio pekee walioingia makubaliano hayo na Serikali na wala siyo mtu mwingine yeyote.

“Nipende kusema tu timu husika itakabidhiwa uwanja siku ya mchezo kwa maana ya Jumamosi ingawa ni kwa kushirikiana na Suma JKT, ila hilo linalozungumzwa kwangu halina mashiko zaidi,” alisema akifafanua hali iliyoonekana kwa baadhi ya makomandoo kupiga kambi magetini kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

Mtumbuka aliongeza wao kama menejimenti wamehakikisha mazingira yote yanakuwa rafiki kuanzia ndani na nje ya uwanja wakitambua kwamba wikiendi hii ni siku muhimu kwa wapenzi na mashabiki wa soka nchini Simba na Yanga.

“Kulikuwa na hali flani ya fangasi katikati ya uwanja kwa maana ya kuna sehemu majani yalikuwa hayaonekani vizuri, jitihada kubwa zimefanyika ili kurudisha ile hadhi yake kwa lengo la timu zetu za Simba na Yanga kuonyesha soka safi,” alifafanua Mtumbuka.

Mbali na Simba ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika itayoshuka uwanjani hapo Jumamosi, Yanga itashuka pia dimbani Jumapili kucheza dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika, ikitoka kupoteza kwa mabao 2-0 ugenini mbele ya US Monastir ya Tunisia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live